DSTV kuanza kuwapa mashavu wasanii wa Tanzania

Wasanii wa filamu na muziki wameshauriwa kuzalisha kazi zenye weledi ili kuweza kushindana na kazi nyingine za filamu na muziki barani Afrika.

Kauli hiyo imetolewa na meneja uendeshaji wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Ronald Baraka Shelukindo wakati akitangaza mikakati ya kuendeleza wasanii wa kitanzania kupitia DSTV .

“Katika kusaidia au kumotivate wasanii wetu, nafikiri nyie waandishi wa habari ni mashuhuda wakubwa,wacheza filamu, wachekeshaji na watu wote ambao wako kwenye sanaa, kwahiyo siku za karibuni mtaona kutakuwa na matangazo ambayo yatawashirikisha wachekeshaji maarufu Afrika,” alisema.

Aidha Lukindo alisema DSTV inakuja na programu nyingi za lugha ya Kiswahili ambazo zinalenga kuwainua wasanii wa kitanzania ili waweze kufika katika hadhi ya kimataifa katika sanaa.
Powered by Blogger.