Mwanzilishi wa kundi la LFLG rapa Billnas ameunga mkono tuhuma za Nuh Mziwanda kwa kumshukia meneja wao Petit Man juu ya uongozi mbaya na upigaji wa hela kupitia mgongo wao.

Billnas akipiga story za eNewz na kusema kuwa matatizo ni kweli yametokea lakini akamshauri Nuh Mziwanda ni vyema kwa sasa wakatafuta namna ya kumaliza mzozo huo.
"Petit ni mmoja kati ya watu wa LFLG, So kama mmoja wetu ana matatizo then wengine wanaweza kutumika kusuluhisha, au vinginevyo anaweza kupunguzwa ili wengine waendelee vizuri na kazi" aliongeza Billnas.
Hapo awali mzozo kati ya Petit Man na wasanii anaowasimamia yaani Nuh Mziwanda na Billnas ulianza kusikika baada ya Nuh Mziwanda kujitoa chini ya usimamizi wa Petii Man kwa madai kuwa ni "mpigaji" na kwamba hutumia majina yao vibaya kupata pesa na pia si meneja anayewajali wasanii wake.

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top