Beki wa klabu ya Manchester United ambaye ni raia wa Ivory Coast, Eric Bailly alipata jeraha baya la goti wakati wa mechi ambayo timu yake ilifungwa 4-0 na Chelsea Jumapili.

39a397fd00000578-3864868-image-a-79_1477244813063
Mchezaji huyo ambaye ana miaka 22 aliumia baada ya kukabiliana na Eden Hazard wa Chelsea.
ALiondolewa uwanjani dakika ya 52.
39a3968500000578-3864868-image-a-87_1477244941472
“Nina wasiwasi kwamba ni jeraha baya,” meneja wa United Jose Mourinho alisema. “Ameumia kwenye goti, eneo lenye kano. Anahisi kwamba ni jeraha baya sana.”
Bailly amechezea United mechi zote walizocheza msimu huu katika mechi za ligi.
Powered by Blogger.