Audio : Kumbe Lolilo Mzizi wa Jiwe ndiye tatizo ya Jay T kuaamua kufanya kazi na R Flow?

Msani Jay T kutoka Burundi mkali wa Lydia, amefunguka kuhusu swala ya kufanya kazi na R Flow huku alikua amepanga afanye na msani maarufu Afrika Mashariki wa Burundi Flava, Lolilo Mzizi wa Jiwe Simba.


..., Tumepanga tufanye nyimbo pamoja
       Baadae ukanigeuka na kuanza kuniomba nikupe pesa elfu Thalathini na tano
      Nikupe pesa wakati muziki haujasonga mbele?
      Bona wengi wao umeimba nawo hawajasonga mbele?
     Naongea na L-O-L_I-L-O my name Jay T ukinifatilia hutaniweza,....

Ni mojawapo ya verse (ubeti) uliyomo kwenye hit single ya msani wa Burundi Fleva, Jay T  iitwayo Message ilitoka baada ya nyimbo Lydia akimshirsha R Flow huku akisema kuwa nafasa ya R Flow wamepanga waimbe na Lolilo baadae akamgeuka ghafla na kuanza kumuomba pesa elfu thalathini na tano (35.000fbu) ili washirikiane.

Wimbo ambao ndani ya takriban miezi kadhaa tangu kuachiwa kwa video yake kwenye Mtandao wa YouTube umetizamwa sana!
 Katika wimbo huo (message), Jay T amejaribu kuvuta hisia na kuwakosowa wasanii maarufu, amejaribu kuvuta picha na namna ambavyo mambo yanavyoweza kutokea kwake binafsi na kwa game ya muziki. 
Jay T amewataka wasani wakubwa wasiwe na lengo ya kubania wengine kwasababu nawo pia wamesaidiwa ili wafike hapo walipo.

"inafikia mpaka sisi wasani chipukizi tunaomba collabo ma braza wetu, ila kuna baadhi ya wengine wanakubali ila hawa wanaojiita wakali wanapenda kutuomba pesa huku wanasahau muziki wetu wa Burundi bado haujatoka. Inasikitisha sana tena ndio sababu ya mi kutunga nyimbo Message ili iwafikie walengwa", amesema Jay T.

Ebu sikiliza kipande cha nyimbo Message uamini mojakwamoja kuwa Jay T akimgusia Lolilo
Powered by Blogger.