Aliyekuwa kocha wa timu ya Azam FC, Stewart Hall raia wa Uingereza amesajiliwa rasmi kuifundisha timu ya AFC Leopards inayoshiriki ligi kuu ya nchini Kenya.

hall-stewart-kocha-wa-azam-fc
Hall amesaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili huku akiwabwaga wapinzani wake waliokuwa wakiwania nafasi hiyo, akiwemo Sam Timbe (Uganda), Didier Homes Da Rosa (Ufaransa), Andrew Mbungo (Rwanda), Patrick Liewig (Ufaransa) na Popadic Dragan kutoka Serbia.
Kocha huyo amewahi kuisaidia timu ya Azam Fc kutwaa kombe la CECAFA Kagame Club Cup mwaka 2015 baada ya kuifunga timu ya Gor Mahia ya Kenya kwenye mchezo wa fainali.
Kabla ya kusajiliwa kwa Stewart, AFC Leopards ilikuwa ikifundishwa na kocha wake raia wa Ubelgiji, Ivan Minnaert aliyefukuzwa kazi mwezi Septemba mwaka huu kutokana na kiwango kibovu kilichokuwa kikionyesha timu hiyo.
Powered by Blogger.