Akaunti za Instagram za Lake FM zahujumiwa, ni za kituo, mkurugenzi na za wafanyakazi wote

Katika kile kinachoonekana kuwa ni hujuma, akaunti ya Instagram ya kituo cha redio cha Lake FM ya Mwanza, imedukuliwa (hacked) Alhamis hii.
doreen-jpg-pagespeed-ce-pafxnhaet5
Kama haitoshi, akaunti ya mmiliki na mkurugenzi wa kituo hicho, Doreen Noni pamoja na za wafanyakazi wote zimepotea pia.
7b02989c-4bf2-4f96-b189-d5213546ceb8
Hujuma hiyo imetokea wakati ambao kituo hicho cha redio kimeaanda show iitwayo Usiku wa Mshike Mshike ya Khadija Kopa na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic itakayofanyika Alhamis hii kwenye ukumbi wa Villa Park Resort.

Akaunti za wasikilizaji na watu wengine waliokuwa wakipromote show hiyo nazo zimepotea. Jumla ya akaunti zilizodukuliwa ni 20. Doreen ameiambia Bongo5 kuwa hiyo ni hujuma ya waziwazi ya maadui wenye lengo la kuwaharibia show hiyo na wanaendelea kuzishughulikia.
Powered by Blogger.