Ajali nyingine Watu watatu wafariki Dunia Tabora

Watu watatu wamefariki dunia na wengine tisa wamejeruhiwa baada ya gari aina ya Noah yenye namba za usajili T739 ASS iliyokuwa ikitokea Nzega kuelekea kata ya Mwantundu wilaya ya Nzega kupasuka tairi ya nyuma kutokana na Mwendokasi.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa sita mchana ambapo waliofariki  wametambuliwa kuwa ni Kadushi Kashimba, Aziza Salome na  Mwanankomi Funuki  wote wakiwa ni wakazi wa Nzega.

Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Itilo wilyaani Nzega ambapo baadhi ya majeruhi wanaeleza hali ilivyokuwa.

Mkuu wa wilaya ya Nzega Godgfrey Ngupula amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Aidha majeruhi hao wanaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya Nzega huku miili ya marehemu ikiwa imehifadhiwa hospiatalini hapo.
Powered by Blogger.