responsive ads

Waziri Simbachawene leo afunguka na kusema Wakaguzi wandani kuweni makini.

Na. Vero Ignatus Arusha.Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Tawala za serekali za mitaa na TAMISEMI George Simbachawene amewataka wakaguzi wa ndani katika  halimashauri hapa nchini kuhakiksha wanasimamia kwa umakini mapato ya halimashauri ili kuchochea chachu ya maendeleo.
Waziri Simbachaweni ameyasema hayo leo hii kituo cha kimataifa cha mikutano (AICC)katika  ukumbi wa Simba katika mkutano wa siku tatu ulioanza leo katika  wa mkutano wa 10  wa wakaguzi wa ndani  ambao uilofanyika jijini hapa ikiwa na lengo la wakaguzi hao wa ndani kuangalia njia muafaka za kukubiliana na changamoto wanazokubiliana nazo.
Amesema kuwa wakaguzi wa ndani katika halimashauri zetu ni watu muhimu sana katika kuangalia hali ya miradi inayoendeshwa na halimashauri kwa maana miradi mingi inafanywa na halimashauri zetu na hivyo kupelekea kuingiziwa pesa nyingi.
Aidha waziri huyo wa TAMISEMI amesema kuwa kwa sasa wameagiza katika halmashauri zote kuhakisha kuwa wakaguzi wa ndani wanakuwa na bajeti yao inayojitegemea tofauti na halimashauri ili kuweza kuboresha hali ya utendaji wao.
Aidha kwa upande wake Raisi wa chama cha wakaguzi wa ndani nchini Tanzania  (IIA)  Richard  Magongo amesema kuwa mkutano huo wa kumi utakwenda sambamba na kushereke miaka kumi tangu kuanzishwa kwa kwa taasisi ya ukaguzi wa ndani.
Amesema kuwa katika mkutano huo wa siku tatu mada mbali mbali zitajadiliwa ambazo kwa kiwango kikubwa kitawqeza kuwasaidia wakaguzi wa ndani katika kuboresha ufanisi wao wa kazi za ukaguzi.
Pamoja na hayo ametoa shukurani kwa Serekali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kusikia kilio chao cha siku nyingi kwa kuweka ofisi
ya mkaguzi mkuu wa ndani Serekalini.
middle 300x250
Powered by Blogger.