responsive ads

Watangazaji redio za mikoani: Wasanii wanatudharau, hawatupi ushirikiano

Kwa muda mrefu sana watangazaji mbalimbali wa redio za mikoani wamekuwa wakiniomba niwafikishie malalamiko yao kwa wasanii wa Tanzania. Jana tu mtangazaji mmoja wa kituo cha Mbeya FM aliniomba nijaribu kulisemea hili.
Radio-Studio-HD-Wallpaper
Lisemwalo lipo na kama linasemwa na watangazaji wengi, basi si la kupuuza katu. Hii imekuwa ikatokea sana kwa watangazaji wa redio hizo pale wanapotaka kufanya interview na wasanii, mara nyingi kwa simu. Wapo ambao huwachukulia kwa uzito na kuongea nao huku wakiwapa heshima ile ile ambayo wanaweza kumpa mtangazaji wa Clouds FM au East Africa Radio.
Mara nyingi baadhi ya wasanii huamini kuwa hizi redio za mikoani zinasikika katika eneo dogo na hivyo hata kama wakifanyiwa interview haiwezi kuwasaidia kwa lolote, haiendi popote. Hii sio kweli kwasababu redio za mikoani zina wasikilizaji wengi ambao ni mashabiki wa wasanii hawa pia.
Zinasikilizwa kwasababu ya licha ya kuzungumzia masuala ya kitaifa, zimekuwa zikiwapa wakazi wa eneo husika habari na matukio yanayowagusa moja kwa moja. Mwananchi aliyepo Ludewa, hawezi kuitegemea Radio One kwa mfano kumpa habari za eneo analoishi, bali anaitegemea redio iliyopo wilayani humo kwa hayo.
Redio za mikoani na wilayani zimekuwa zikifanya kazi kubwa kupromote kazi za wasanii, hivyo watangazaji wake wanahitaji kupewa uzito sawa kama ambavyo wasanii huwapa wale waliopo Dar es Salaam.
Wasanii wanapaswa kuwapa ushirikiano watangazaji hawa kwasababu kazi wanayofanya ni kuzicheza nyimbo zao na kuwaongezea mashabiki, wanapaswa kuwachukulia kama marafiki zao muhimu. Mashabiki wa wasanii hawa wana haki ya kuwasikia wasanii wanaowapenda wakihojiwa pia kwenye redio za maeneo yao.
Nafahamu kuwa redio kwa sasa zimekuwa nyingi na hivyo wasanii hujikuta wakipokea simu kibao za interview hadi kuwachosha kuongea na kuhitaji kupumzika. Huwachosha zaidi kwakuwa mara nyingi huulizwa maswali yale yale. Lakini watambue kuwa wao ni watu maarufu na kuhojiwa na waandishi na watangazaji ni sehemu muhimu katika career zao, hawawezi kukwepa. Wanapaswa kuwachukulia watangazaji wa redio zote kwa usawa.
middle 300x250
Powered by Blogger.