Video : Mkubwa Fella aonyesha Nyumba Mpya 4 Za Yamoto Band

Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe ambaye pia ni mmiliki wa Yamoto Band,
Said Fella alitambulisha kwa waandishi nyumba mpya wanatakazomiliki
bendi yake hiyo zilizopo Mbande-Kisewe jijini Dar.


Akizungumza na mtandao huu mara baada ya kuzitambulisha nyumba hizo,
Fella alisema kuwa kila mmoja atakabidhiwa hatimiliki yake na kwamba ni
nyumba zinazojitegemea.


“Kama uonavyo, nyumba zipo nne kwa Yamoto ambazo zote zinafanana hadi
ndani. Ukiingia kuna master, vyumba viwili. Eneo la kulia chakula, jiko
na sebule kubwa,”
alisema Fella.
Powered by Blogger.