Ushindi wao wa 1-0 uliwawezesha kufuzu kwa fainali zitakazochezewa Gabon mwaka ujao kama mojawapo wa mataifa mawili bora yaliyomaliza ya pili katika makundi.
Wapinzani wao Kundi D Burkina Faso pia walifuzu kwa ushindi wa dakika za mwisho wa 2-1 dhidi ya Botswana, ushindi uliowawezesha kuongoza kundini.
Tunisia na DR Congo pia zilifuzu baada ya kuongoza katika makundi yao.
Mataifa 16 yatashiriki michuano hiyo itakayoandaliwa 14 Januari hadi 5 Februari. Waliofuzu ni viongozi wa makundi yote 13, mataifa mawili bora yaliyomaliza ya pili hatua ya makundi, na wenyeji Gabon.
Algeria, Cameroon, Egypt, Ghana, Guinea-Bissau, Ivory Coast, Mali, Morocco, Senegal na Zimbabwe walijihakikishia nafasi kabla ya mechi za Jumapili.
Katika kufuzu, Uganda pia walifikisha alama 13, kupitia bao la dakika ya 35 la Farouk Miya mjini Kampala, lakini wakaorodheshwa wa pili kwa sababu walilemewa na Burkina Faso klabu hizo mbili zilipokutana.
Mara ya mwisho Uganda kucheza fainali za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika ilikuwa miaka 38 iliyopita ambapo walimaliza wa pili baada ya kushindwa fainali an Ghana.

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top