Jioni ya September 3 2016 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ndio ilihitimisha safari yake ya kuwania kucheza michuano ya mataifa ya Afrika 2017 maarufu kama AFCON, Taifa Stars iliyokuwa Kundi G lenye timu za Misri, Nigeria na Chad ambao walijitoa, imecheza mchezo wake wa kukamilisha ratiba dhidi ya Nigeria Super Eagles.
Taifa Stars ambayo ilicheza mchezo huo wa Kundi G kukamilisha ratiba sawa na Nigeria, imekubali kipigo cha goli 1-0, goli  ambalo lilifungwa dakika ya 77 na nyota wa Nigeria anayeichezea Man City ya England Kelechi Iheanacho, hiyo ni baada ya kuishambulia Taifa Stars kwa muda mrefu.Mchezo wa kwanza wa Taifa Stars dhidi ya Nigeria ulichezwa September 5 2015 uwanja wa Taifa Dar es Salaam na ulimalizika kwa suluhu ya 0-0, hiki ni kipigo cha 5 Taifa Stars kufungwa na Nigeria katika mechi zake nane walizowahi kukutana, Taifa Stars haijawahi kuifunga Nigeria na wameambulia sare 3 kati ya mara 8 walizokutana.

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top