Snura afunguka kwanini muziki wake umechelewa kwenda kimataifa,sababu hii hapa..

Msanii wa bongo fleva ,Snura hivi karibuni amepata show yake ya kwanza nchini Afrika kusini licha ya kuwepo kwa muda kwenye muziki.
Akiongea kwenye kipindi cha Enewz cha Eatv ,Snura amesema alikubali kwenda kufanya show hiyo nje ya nchi kwa sababu ilikuwa na maslahi,na kuongeza kuwa alikuwa hataki muziki wake uende kimataifa kwa ajili ya sifa tu bali umlipe ndio maana alichelewa kuvuka mipaka.
Ni kweli kiasi cha pesa walichonilipa Afrika kusini ni tofauti sana,yaweza kuwa ndio maana mimi nilichelewa kwenda kimataifa kwa sababu mimi nachukulia kama kazi hata kama naenda nje ya nchi nisiende kisifa kwamba nionekane tuu nimenda,nilitaka niende kwa masilahi na nilikuwa naamini ipo siku watanielewa na watatoa kile nachokitaka” alisema Snura.
Powered by Blogger.