Real Madrid na Atletico Madrid zafungiwa na FIFA kufanya usajili hadi January 2018

Klabu za Real Madrid na Atletico Madrid zinazoshiriki ligi ya Hispania, hazitaweza kusajili wachezaji kwa madirisha mawili ya usajili yajayo kufuatia FIFA kukataa rufaa yao waliyoikata juu ya kufungiwa kufanya usajili.
zidane-simeone
Mwezi Januari mwaka huu kamati ya nidhamu ya FIFA ilitangaza kuzifungia klabu hizo zisifanye usajili katika madirisha mawili yajayo kwa kosa la kuvunja sheria za usajili waliposajili wachezaji chini ya miaka 18 wasio wahispania lakini adhabu hiyo haikuanza kufuatia timu hizo kukata rufaa na hivyo wakaweza kufanya usajili katika dirisha hili lililofungwa hivi karibuni.
Hivyo baada ya rufaa zao kukataliwa miamba hiyo ya Hispania itaweza kusajili wachezaji wapya Januari,2018 na Atletico Madrid wanatakiwa kulipa faini ya pauni 622,000 na Real Madrid watalipa faini ya pauni 249,000. Lakini Real Madrid wamesema kuwa sasa wanaenda kukata rufaa ya katika mahakama ya michezo .
Aidha klabu hizo zinaweza kusajili wachezaji lakini wasiwatumie. Barcelona April 2014 waliwahi kufungiwa kutokana na kufanya kosa kama hilo na adhabu yao iliisha Januari 2016, waliwanunua Arda Turan na Aleix Vidal mwaka 2015 lakini hawakuwatumia mpaka adhabu ilipoisha.
Powered by Blogger.