Rais John Magufuli leo ametishia kubadilisha noti kama njia ya kuwadhibiti watu wanaodaiwa kuficha fedha majumbani.


Alitoa kauli hiyo katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Alhamis hii jijini Dar es Salaam.
Alisema lengo lake ni kutaka kuwadhibiti watu wanaodaiwa kuficha fedha.
Alisema kwa mamlaka aliyonayo anaweza kuamua kubadili fedha ili zile zinazofichwa na watu hao wakose mahali pa kuzipeleka.
“Katika utawala wangu fedha za bure hazitakuwepo kwa sababu zilizokuwepo awali zilitokana na fedha za wizi kutoka serikalini ambazo kwa sasa zimedhibitiwa, kwa mwendo ninaokwenda nao sasa ni ngumu kwa mwananchi kupata fedha bila kufanya kazi,” alisisitiza Dk Magufuli.
Powered by Blogger.