Amesema hawezi kushirikiana na Rayvan, kwa kuwa wote wako "level" ya kimuziki na wana mashabiki sawa, kwahiyo hakutakuwa na kipya, na kwamba ni bora akafanya na msanii mkubwa kuliko yeye.
Akipiga story ndani ya eNews amesema “Colabo ni kubadilishana mashabiki kwa wakati nafanya colabo na Diamond nilikuwa nikilenga mahali ambapo muziki wa Diamond umefika na pia kwa kuwa Diamond ana'hit' nyingi kwa hiyo likuwa ni mpango wa kufikisha muziki wangu mbali”
Ameendelea kusema kuwa haogopi kufanya collabo na Raymond, isipokuwa hiyo ni mipango aliyonayo anayoamini itamuwezeshakupiga hatua
“Ningekuwa naogopa colabo basi ningeogopa kufanya colabo na Diamond kwa kuwa ni muimbaji mzuri kuliko Rayvan lakini niliamua kukaza tu ili kufika mbali, lakini pia inabidi tupate muda tutengeneze wimbo mzuri ili kitoke kitu kizuri”. Aliendelea kusema Harmonize.
Pia hakusita kuelezea maswala ya mahusiano yao na Wolper akisema “siku zinavyozidi kwenda binadamu anapata mawazo mapya pamoja na kukua lakini pia nafikiri ilikuwa ni upya ndiyo maana kila siku tulikuwa tukifanya mambo mbalimbali kwa kuwa wote tulikuwa tukitamaniana".

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top