Msanii wa Kenya alalamika kuzinguliwa na Linex,kisa?

Msanii wa Kenya anayejulikana kama Bahati amelalamika kuzinguliwa na Linex baada ya kutotokea kwenye video ya nyimbo yake ambayo amemshirikisha.
Akiongea na Planet Bongo,msanii huyo ameonyesha kusikitishwa na kitendo cha Linex kilimchomgharimu pesa baada ya kukodi hoteli kwa ajili yake lakini Linex hakuonekana.
Linex sijui ni msanii wa aina gani, tumepanga video kila kitu nimeboook hadi hoteli, akazingua last minute, unajua muziki at the same time tunafunguliana milango, na mimi nilikuwa nataka hii nyimbo iwe ya Linex kuingia Kenya, kwa hiyo alikuja Kenya nikampa verse akaenda poa, tukapanga video, alianza kunipa excuse kwamba meneja hajabook, na yeye ndiye aliyekuwa akiniambia tupange shoot, unajua mi sasa hivi nimewin three times top male artist, sa hii ingekuwa kwa ajili ya yeye kuingia Kenya”,alisema Bahati.
Linex alipoulizwa kuhusu suala hilo alifunguka na kusema, “Kilichotokea ni kwamba nilishindwa kufika kwa sababu mi nakumbuka tumepanga tufanye kazi Jumamosi, mi nikapata kazi ilikuwa inafanyika siku ya Ijumaa, kwa hiyo nikawa na hakika kwamba kwa kuwa imekuwa hivyo, itabidi nipige tu flight asubuhi kabisa, management yangu haikunifanyia booking ya tiketi kwa hiyo nikashindwa kusafiri hiyo Jumamosi kwenda kufanya hiyo video
Powered by Blogger.