Msanii mkongwe wa muziki, Mwasiti Almas amefunguka na kueleza kwanini wasanii wapya kama akina Vanessa Mdee wanafanya vizuri zaidi sasa kuliko kizazi chao.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Unaniangalia’ amedai wasanii wengi wa sasa wamekuja katika muda mzuri zaidi tofauti na wakati wao.
“Kizazi changu mimi sikuwa na akina dada Jide,” Mwasiti aliliambia gazeti la Mtanzania. “Hivyo kizazi cha akina Vannesa Mdee hakiwezi kufanana na cha kwetu. Lazima kuwepo na utofauti, lakini pia hawa wa sasa wamekuja kupata muda mzuri zaidi tofauti na muziki wa miaka ya nyuma,” alifafanua Mwasiti.
Mwasiti amewahi kutamba na wimbo wa ‘Nalivua Pendo’ ambao mwaka 2009 ulipata tuzo ya Wimbo Bora wa Zuku Rumba katika Tuzo za Kili.
Powered by Blogger.