Msanii Dogo Janja amesema saa hivi ana mpango wa kuweka muonekano wake vizuri kibiashara zaidi, ili aweze kuingiza mkwanja mrefu zaidi ya muziki anaofanya.

Akizungumza  mishe mishe media, Dogo Janja amesema sasa hivi muonekano wake umebadilika kutokana na kukua, na pia kutokana na jinsi anavyojiweka safi, ili aweze kuvutia makampuni kumpa dili mbali mbali za biashara.
"Kikubwa ambacho naangalia sasa hivi ni brand yangu, pia msanii msanii kuwa na muonekano mzuri unaweza kupata dili za matangazo, ndio maana some times napendeza unaweza kukuta nafanya tangazo, naweza nikatumika kama artist, naweza nikatumika kama model, naweza nikatumika kama yeyote kutokana na muonekano wangu, na apearance yangu ambayo siku hizi nimekuwa, na imekuwa nzuri hadi mwenyewe najijua kabisa kama napendeza", alisema Dogo Janja.
DogoJanja ambaye kwa sasa ameachia video yake mpya ya 'kidebe', amesema kitendo hicho kitamsaidia kuingiza pesa zaidi, huku akikiri kukua huko kumemsaidia kuongeza upana wa mawazo yake katika kazi zake, tofauti na siku za nyuma.
Powered by Blogger.