TANGAZO
Mwanamuziki Likiliki Francis almaarufu kama Omario Lee kutoka Burundi mwenye makazi yake nchini Uganda anatarajia kuachia track mpya katika studio Fresh Vybz Studio  chini ya mikono ya Producer Lexlogic, track itakuja kwajina la Hema Water ambayo ni jina la Kampuni inayo usika na Usambazaji wa Maji nchini Uganda pia tayari Msani Omario Lee amekwisha saini mkataba na Kampuni hiyo.

Baada ya kutamba na nyimbo zake kadhaa kama Coca-Cola aliyoshirikiana na Yuda, Yeye aliyo mshirikisha Micho pamoja na Who are you love,  anazidi kufanya vizuri na kuitangaza Burundi Fleva nchini Uganda mjini Kampala.

Tayari ameanza kukubaliwa na wanamuziki wakubwa nchini hapo na hivi karibuni ameiambia Africanmishe kuwa anatarajia kungia studio akishirikiana na mwanamuziki kongwe mwenye sifa nyingii Afrika Mashariki, hata hivyo hakupendelea kumtaja jina.

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top