Mmwanamuziki Hassan almaarufu kama Arobazz kutoka Burundi mwenye makazi yake nchini Kenya amealikwa na mwanamuziki kongwe wa Kenya Nonini kwenye sikukuu ya kuzaliwa kwake hapo Novemba, 01, 2016 mjini Nairobi.

Baada ya kufanya vizuri na nyimbo yake mpya (Mimi Na Wewe) akimshirikisha Black G, anazidi kutamba na kuitangaza vyema Burundi Fleva nchini Kenya. Akizungumza  na Mishe Mishe , Arobazz amesema na kutangaza nyimbo yake mpya itakayo achiliwa hivi karibuni.

Arobazz
" kwasasa nazidi kuendelea vizuri na nafurahi kuona wakenya wanazidi kupenda kazi zangu, kwasasa nimealikwa na msanii mkubwa Afrika Mashariki ambaye ni Nonini kwenye sikuku ya kuzaliwa kwake, kuna nyimbo mpya natarajia kuiachia ivi karibuni ipo chini ya mikono ya Producer Sulex kwasasa yupo kenya na ninaimani, nyimbo yangu hii mpya itasikika kwa mara ya kwanza kwenye Show hiyo ya Nonini hapo Novemba tarehe moja, watakao udhuria ndiyo watabahatika kuisikia"amesema Arobazz

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top