Mrembo Divine amekubali kuigiza filamu na kampuni la Tambwe The Great Filams

Tambwe ( kiongozi wa Tambwe the Great Filams na mrembo Divine) 
Kampuni la kuigiza filamu nchini Burundi ijulikanayo kama Tambwe The Great Filams inazidi kuleta upinzani mkubwa katika soko la filamu Afrika Mashariki, baada ya kutangaza filamu yao mpya ambayo itaachiwa hivi karibuni.

Katika Filamu mpya hiyo msanii Jay Fire atakuwepo ndani pia Kampuni hiyo imetangza kuwa na makubaliano kati yawo na mwanadada mrembo aitwaye Divine, ambaye wengi wanamfahamu kwenye clip video nyingi za wanamuziki wa Burundi.
Staa huyu mrembo wa Burundi, Divine tayari amekwisha kamilisha makubaliano ya kuigiza katika filamu mpya ambayo  Kampuni Tambwe The Great Filams ya nchini Burundi inaanda, ma staa wengi tayari wameanza kuvutiwa na Kampuni hiyo ya kuigiza filam nchini Burundi.
Jay Fire na Mrembo Divine
Baada ya kupata tarifa kuwa msanii Jay Fire ataigiza kwenye filamu hiyo, tumejaribu kumtafuta kiongozi wa kundi hilo na amethibitisha kuwa mrembo Divine ambaye wengi wanapendelea kumuona kwenye video clip nyingi, tayari amekubaliana na kampuni  hiyo kwa kuigiza filamu akiwa chini ya mkataba na Tambwe The Great Filams.

Divine ni binti mrembo anaye vutiwa na kila mwanaume kwa urembo Mungu amemjalia, basi itakuwa ni fursa kubwa kuonesha kipaji chake katika uigizaji kwasababu ana kila vigezo vya kumfanya mpenzi wa filamu kutizama filamu ambayo mrembo Divine akiwemo.


Powered by Blogger.