Mkali wa wimbo ‘Hainaga Ushemeji’ Man Fongo anajipanga kwenda Afrika Kusini kushoot video ya wimbo wake mpya aliyomshirikisha Chege Chigunda.

Muimbaji huyo akiongea na kuluti mc mwandishi wa tovuti hii amesema video hiyo atashoot katika mji wa Soweto Afrika Kusini kutokana na mji huo kuendana sambamba na mazingira ya muziki anaofanya.
“Ngoma yangu ya tatu ambayo nitaimba na Chege hii kidogo nitasafiri kwenda Soweto,” alisema Man Fongo. “Mji wa Soweto ni mji ambao umekaa na mazingira ya kimtaani mtaani , na muziki wangu wa singeli ni muziki wa uswahilini, kwa hiyo nikisema nikashoot Cape Town au Durban nitakuwa nadanganya,”
Muimbaji huyo kwa sasa ameachia wimbo mpya ‘Kibaka’ huku akidai video itatoka siku chache zijazo.
Powered by Blogger.