Mark Zuckerberg ambaye ni Mmiliki wa Facebook sasa ni tajiri namba 5 duniani

Facebook, Instagram na WhatsApp ni app tunazozitumia zaidi kwa sasa. Na tena tukizungumzia WhatsApp, ni kitu kinachotuchukulia muda mwingi zaidi kuliko kitu kingine chochote kwa sasa.
zuckerberg-1940x1164
Vyote hivi ni mali ya Mmarekani kijana asiye na makuu, Mark Zuckerberg. Hivyo si jambo la kushangaza ukiambiwa kuwa anakwea kwa kasi kutaka kumpokonya Bill Gates nafasi yake ya kwanza kama mtu tajiri zaidi duniani.
Kwa mujibu wa Forbes Zuckerberg anashika nafasi ya tano sasa akiwa na utajiri unaofikia dola bilioni 54.5.
Zaidi ya Bill Gates mwenye utajiri wa dola bilioni 78.6, Mark anazidiwa na Amancio Ortega (68.3 B), Warren Buffett ($67.7 B) na Jeff Bezos ($66.7 B).
Pamoja na utajiri huo, Mark aliahidi kuwa atatoa 99% ya share zake za Facebook kusaidia mambo ya kijamii.
Powered by Blogger.