Kituo cha redio cha Magic FM,kuja na muonekano na vipindi vipya

Kituo cha redio cha Magic FM, kinachomilikwa na kampuni ya Afrika Media Group kinatarajia kuzindua muonekano mpya wa redio hiyo Septemba 26 mwaka huu samabamba na uboreshaji wa vipindi baada ya kutorusha matangazo yake takribani siku 26 .
dsc02400
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa vipindi, Orest Kawau, amesema muonekano wa kituo hicho umetokana na maoni ya wasikilizaji kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo masafa ya redio yanawafikia katika mkoa wa Mwanza, Dar es Salaam, Arusha, Morogoro pamoja na Tanga.
“Baada ya utafiti wetu kutoka kwa wadau wetu kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania, tumeboresha vipindi vyetu na tumekuja na mkakati mpya wa kuendelea kuwapatia burudani na habari zenye uhakika zaidi kama ilivyokuwa ada yetu,ninachowasihi ni kuendelea kusikiliza Magic FM kwa popote pale ulipo kupitia frequency zetu katika mikoa ambayo tunapatikana lakini pia kwa wale ambao mpo nje ya Tanzania kupitia tune in mnatupata ukiwa eneo lolote duniani,” alisema Kawau.
Miongoni mwa vipindi vilivyofanyiwa marekebisho ni kipindi cha Morning Magic kinachorushwa kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa nne, na kipindi kinachoruka kuanzia sa kumi mpaka saa kumi na mbili, pamoja na kile cha michezo na Magic kinachorushwa saa 2 mpaka saa 3 usiku.
Powered by Blogger.