Inter Star, Lydia Lidic Academic inazidi kuwa kileleni, Vitalo inazidi kudidimia kwenye Ligi Kuu, Primus Ligi

Ligii kuu Primus Ligi imeingia kwenye wiki yake ya pili, tayari timu kadhaa zinazidi kuonesha ubabe wao na zingine timu ambazo zimepewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri msimu huu zinazidi kudidimia.
Timu ya Inter Star inazidi kufanya vizuri baada kuonekana  kama kikosi chao ni kibovu ila kwasasa inazidi kuwarejesha mashabiki zao baada ya kutokufanya vizuri msimu uliyo pita.

Inter Star na Lydia Lidic Academic inazidi kuongoza kileleni mwa Ligi Kuu, zinafikisha pointi 6 baada ya mechi mbili uku wabingwa watetezi, Vitalo FC inazidi kudidimia kiasi kikubwa ikiwa na pointi moja tu katika mechi mbili.

Inter Star imeeneza pointi zake zote sita baada ya kujielekeza Mkoani Ruyigi na kuicharaja vibaya Flambeau de L'Est bao moja kwa mbili ya Inter  Star, Lydia Lidic Academic imepata ushindi wao ugenini kwa tabu ya bao moja bila dhidi ya Ngozi City, Aigle Noir ikiwa nyumbani Makamba imepata ushindi wa bao moja bila na kuwa na pointi nne katika mechi mbili, Les Lieres ikiwa Bujumbura  imepata ushindi wa bao tatu bila dhidi Rusizi FC, Messager Bujumbura imepata kichapo ya mabao mawili dhidi ya Muzinga na upande mwingine wabingwa watetezi Vitalo wameridhika kwenda sare ya kutokufungana dhidi Olympic Star  na pia Musongati imekwenda sare ya mbili mbili dhidi Magara.

Messager  buja 0-2 Muzinga
Aigle noir 1-0 buja CTY
Musongati 2-2 Magara
Flambeau 1-2 Inter star
Ngozi city 0-1 LLB
Olympic star 0-0 Vitalo
Les lierres 3-0 Rusizi 

Picha chache za mechi ya wiki ya pili Ligi Kuu Primus Ligi
Les Lieres vs Rusizi

Madame Les Lieres na kamanti yake wakifurahia ushindi wao wa kwanza
Muzinga vs Message  Buja
Powered by Blogger.