responsive ads

Hawa ndio wachezaji 10 wanaolipwa mishahara mikubwa Ligi kuu Tanzania msimu wa 2016/2017

Hii ndio Orodha ya wachezaji 10 wanaolipwa mishahara mikubwa Ligi Kuu Tanzania msimu huu wa 2016/2017:

1.  Serge Wawa, ni beki wa kati wa Azam FC, mwenye asili ya Ivory Coast , analipwa dola za kimarekani elfu  7 sawa na miliomi 15 za kitanzania. Tuwakumbushe kuwa Wawa amefanya vizuri na kuipa heshima  ya ubingwa wa CECAFA Kagame Cup  klabu yake ya Azam FC.

2. Obrey Chirwa, ni mshambuliaji  wa zamani wa FC Platinium, raia wa Zambia na amesajiliwa na  Yanga kwa dau la dola  1.00.000  za kimarekani ni sawa na shilingi  milioni 200 huku anapewa mshahara wa milioni 10 kila mwezi.

3. Donald  Ngoma , mshambuliaji wa Yanga SC  anaingiza milioni 7.6 kila  mwisho wa mwezi.

4. Tambwe Amissi, mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania msimu uliyo pita raia wa Burundi mchezaji wa Yanga SC naye pia anaingiza milioni 7.6 za kitanzania  kwa mwezi.

5. Haruna Niyonzima,  Kiungo wa  kimataifa wa Rwanda, mchezaji wa Yanga SC  naye pia anaingiza milioni 7.6 za kitanzania kwa mwezi.

6. Vicent Bossou,  ni beki wa Yanga  amejiunga na klabu hii akitokea Korea  Kusini katika klabu Goyang Hi  FC naye pia anaingiza milioni 7.6 za kitanzania.

7. John Bocco, mchezaji wa  Azam FC huku naye anaingiza milioni 5 za kitanzania kila mwisho wa mwezi.

8. Laudit Mavugo, mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, kwasasa Laudit anakula  mshahara wa dola za kimarekani  2000 sawa na milioni 4.3 za kitanzania.

9.  Juuko  Murshid,  Beki wa kimataifa wa Uganda pia mchezaji wa Simba  SC, ameisaidia timu yake ya taifa kufuzu kombe la mataifa ya Africa mwakani nchini Gabon  baada ya miaka 38, beki huu anakula  milioni 3.2 kila mwezi.

10. Vicent  Atchouailou De Paul Angban, kipa wa Simba raia wa Ivory Coast, anaridhika na dola 1000 za kimarekani sawa na milioni 2.1 za kitanzania.middle 300x250
Powered by Blogger.