Bizimana Hassan ameumia katika mechi dhidi ya Bujumbura City

Mshambuliaji wa timu ya taifa Intamba Murugamba pia wa klabu ya Mkoani Makamba Aigle Noir FC, Bizimana Hassan ameumia usoni baada ya kugongana na beki wa klabu ya Bujumbura City kwenye mechi ya Primus Ligi katika wiki yake ya pili.
Bizimana Hassan ameifungia bao moja pekee iliyo patishia ushindi na kuondoka na pointi tatu timu yake mpya Aigle Noir  ambayo amejiunga msimu huu akitokea Inter Star.

Bizimana Hassan ameumia na vipimo vimeonesha kuwa tatizo hilo sio kubwa sana baada ya kuumia kwa kupelekwa nje katika mechi hiyo  na kuweka mashaka kwa mashabiki wa klabu hiyo.
 Daktari wa klabu hiyo amethibitisha kuwa tatizo sio kubwa sana ila analazimika kupata matibabu  ya nguvu ili kuweza kunusuru kipaji chake cha soka na kutowa mashaka kwa mashabiki wa timu hiyo ambayo baada ya mechi hapo wengi wameanza kusema, pengine mshambuliaji wao anaweza kaa nje ya uwanja miezi kadhaa.
 Itakuwa ni pengu kubwa endapo Aigle Noir FC itaweza kumkosa mshambuliaji Hassan ambaye ni kijana mwenye kipaji cha aina yake  lakini hawana nanma ingawa wataukosa mchango wake katika mechi watakayo shiriki hadi atakapopona.

Tuwakumbushe tena Bizimana hassan amejiunga na Aigles Noir msimu huu akitokea Inter Star inayo shiriki daraja ya kwanza na aliweza kuonyesha makali kwenye baadhi ya mechi na kumaliza msimu akiwa mfungaji bora wa klabu yake Inter Star.

Powered by Blogger.