Baada ya kuzushiwa kifo, Bilionea Dangote ameyaandika haya.
Bilionea
namba moja barani Afrika, Aliko Dangote amekanusha uvumi unaosambaa
kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia akiwa nchini Ujerumani.
Taarifa
hizo zinaeleza kuwa bilionea huyo amefariki akiwa nchini Ujerumani
baada ya kuugua kwa muda mfupi. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa
familia ya bilionea huyo imethibitisha kifo cha ndugu yao huyo na kusema
kuwa ni pigo kubwa kwa Afrika.
Kupitia
ukurasa wake wa Twitter, Dangote ameandika hivi “I am hale, hearty and
alive. Please disregard malicious report saying otherwise. Thank you.” ,
akimaanisha kuwa yeye ni mzima wa afya na kuwataka watu kupuuzia
taarifa zinazoeleza kivingine.”
Akimaanisha “Mimi ni mzima na buheri wa afya. Tafadhali puuzeni taarifa zote zinazosema vinginevyo. Asanteni.”