responsive ads

Timu zaidi ya mbili zinanihitaji - Harerimana Moussa Hapfizi

Mchezaji wa timu ya taifa Intamba Murugamba pia wa klabu DCMP ya DR Congo,  Harerimana Moussa Hapfizi ambaye kwasasa yupo nchini mwake Burundi mda mrefu uku akiendelea mazoezi katika timu ya Inter Star ambayo ndiyo timu yake iliyo mtambulisha kimataifa zaidi.

Mashabiki wa Inter Star na baadhi ya watu wameanza kufikiri kama kiungo uyo wa DCMP anaweza kuichezea Inter Star kwa mara nyingine tena ila mchezaji Hapfizi hakuwa wazi zaidi na swala hilo.
Harerimana Moussa Hapfizi amesema kuwa kuna timu zaidi ya mbili zinamuhitaji ila amekataa kuzitaja jina  na kutuhaidi siku chache  tutatambua ni timu gani kama ni ya nje ya nchi ao ya nchini.

"Ndiyo unajua unapo kuwa likizo mi kama mchezaji siwezi kaa chini bila kufanza mazoezi, ndiyo maana nimeamua kufanza katika timu yangu ya Inter Star ila sijawa mchezaji wa Inter Star, manager wangu bado anajadili na timu yangu ya DCMP kwa kuweka sawa ila kuna timu mbili zinanihitaji na siwezi kuzitaja  kwasababu mambo bado, ninaimani mtakuja kutambua baadae". Amesema  Harerimana Moussa Hapfizi.

kwasasa kiungo  Harerimana Moussa Hapfizi anaendelea vizuri na pia ameanza mazoezi katika kikosi kitakacho wakilisha Burundi nchini Niger kwa mechi ya kuwania kufuzu kombe la Can2017.

middle 300x250
Powered by Blogger.