TIMU YA CHELSEA YAWEKA MEZANI PAUNI MILIONI 32 KUMREJESHA DARAJANI BEKI DAVID LUIZ

Chelsea imepeleka maombi ya kuduwaza ya kutaka kumsajili beki wake za zamani David Luiz kwa pauni milioni 32. Hiyo inakuja ikiwa ni miaka miwili tangu Chelsea wamuuze Mbrazil huyo kwenda PSG kwa dau lililovunja rekodi ya mabeki duniani - pauni milioni 50. Chelsea wanahaha kusaka sentahafu baada ya juhudi zao za kutaka kumsajili Alessio Romagnoli wa AC Milan na Kalidou Koulibaly wa Napoli kukwama.
Powered by Blogger.