Kituo cha Radio 5 FM na Magic FM zafungiwa kwa muda usiojulikana

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametangaza kuvifungia kwa muda usiojulikana vituo viwili vya Redio kurusha matangazo yao.
Waziri Nape ametangaza uamuzi huo hivi punde katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kuzitaja redio hizo kuwa ni Radio 5 FM ya Arusha na Radio Magic FM ya jijini Dar es Salaam.
“Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo (Agosti 29 2016) hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake,” alisema Nape.
Amesema redio hizo kwa nyakati tofauti na katika vipindi vyao tofauti walitangaza habari zilizokuwa na uchochezi ambazo zinaweza kuvuruga amani ya nchi.
Aidha Nape amesema amewasiliana na kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kuwahoji wahusika na kisha kushauri adhabu ambazo zitakazofaa dhidi yao.
Source: Habari Leo
Powered by Blogger.