Neeskens Kebano raia wa DR Congo amejiunga na Fulham ya Uingereza

 Baada ya msimu mmoja tu ameutumia vizuri na KRC Genk ( Ubeljiji D1), kiungo kijana wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Neeskens Kebano amejiunga rasmi na Fulham ( Uingereza D2) kwa mjibu wa klabu hiyo ilivyo tangaza  Ijumaa kupitia tovuti yake rasmi.

Mwenye umri wa miaka 24, Kebano amesaini mkataba kwa kipindi cha misimu mitatu pamoja na chaguo. Ada ya uamisho wake inakadiriwa kwa Euro milioni 4.5 na milioni moja ya ziada (bonus) kama timu itapanda daraja la kwanza.

Kebano amefunzwa katika klabu ya PSG, kwa mara yake ya kwanza ameichezea timu ya taifa ya Ufaransa ya vijana kabla ya kuchukuliwa na timu ya taifa ya DR Congo mwaka 2014 ambapo amesaidia nchi yake kupata nafasi ya tatu katika mashindano ya Kombe la afrika nchini Equatorial Guinea mwaka 2015.

Tuwakumbushe kuwa Kebano atapata fursa ya kubadilika msimu huu ambapo atashirikiana na wachezaji wengi wa Afrika kama Craven Cottage, mshambuliaji wa Nigeria Sone Aluko na pia mshambuliaji nyota wa Togo  Floyd Ayité.
Powered by Blogger.