Muongozaji wa video nchini, Msafiri wa kampuni ya Kwetu Studios, ametaja sababu zinazowafanya waongozaji wa wasanii kusafiri hadi Afrika Kusini kushoot video zao.

14032839_398193157017949_716670172_n
Akiongea na mtangazaji wa Jembe FM, Natty E, Msafiri alisema kikubwa na muhimu ni kutafuta exposure katika kazi zao. Anadai akienda huko hukutana na watu ambao hajawazoea na kutengeneza connection muhimu huku pia akijifunza njia tofauti za kufanya muziki.
Amesema sababu nyingine ni upatikanaji rahisi wa location, models na vitu vingine muhimu kuliko ambavyo kwa Tanzania vina mlolongo mrefu. Amesema kama unataka kutumia kitu au sehemu ya kawaida tu kwenye video, itakulazimu kuzunguka BASATA, bodi ya filamu na mamlaka zingine ili kupewa kibali.
Ameongeza kuwa kwa Afrika Kusini kama msanii anataka kutumia nguo za polisi huandika barua moja tu na hujibiwa siku hiyo hiyo na kuanza kazi. Msikilize hapo chini.
Powered by Blogger.