Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Joto la Asubuhi cha EFM, Gerald Hando amefunga ndoa Jumamosi hii na mwanadada aitwae Miriam Kitenge.

AAA
Mr & Mrs. Gerald M. Hando.
Ndoa hiyo ambayo ilihudhuriwa na ndugu jamaa pamoja na marafiki, ilifanyika katika ukumbi wa Golden Tulip Posta jijini Dar es salaam.
Mtangazaji huyo amewashukuru ndugu pamoja ambao walishiriki kwa namna moja katika kufanikisha shughuli hiyo.
“Hatujalala, muda huu mimi na mke wangu tungependa kukushukuru wewe ndugu jamaa rafiki kwa ushiriki wako. Uwe wa mawazo wa maneno na hata wa vitendo katika kufanikisha sherehe za harusi yetu. Hakika tumefarijika Sana. Tunasema asante sana, Mwenyezi Mungu akuzidishie na tukutakie usiku mwema,” alianda Gerald Hando kupitia instagram yake.
Powered by Blogger.