Msanii wa Bongo Freva Ruby: Afunguka na Kusema Sikwenda Fiesta sababu maslahi ni ‘kiduchu’, atangaza vita na waliomtoa

Muimbaji wa ‘Na Yule’ Ruby amesema hakwenda Mwanza kutumbuiza kwenye Fiesta licha ya ‘kusajiliwa’ kwenye msimu mpya wa tamasha hilo maarufu, kwasababu waandaji hulipa fedha ‘kiduchu.’
ruby1
Kauli yake inakuwa mkuki kwenye moyo kwa Clouds FM ambao ndio waliomfikisha hapo alipo kwa kukivumbua kipaji chake.
Akiongea na tovuti ya Tizneez, Ruby alidai kuwa kutolewa kimuziki na Clouds Media, hakumaanishi kuwa ataendelea kuwatumikia kama wanavyotaka kwakuwa naye ana maisha yake kwa sasa.
“Kisa ni Clouds ndio nisiwe free na kuongea?” alihoji muimbaji huyo ambaye kwa miaka mingi sauti yake imekuwa ikisikika kwenye matangazo kibao ya kituo hicho maarufu cha redio nchini. Amedai kuwa show ya Fiesta ni kubwa kuliko maslahi wanayolipa na kwamba yangemwacha katika wakati mgumu kuandaa show yake.

Anadai kuwa hahofii vita yoyote na kituo hicho chenye nguvu kilichowahi kuingia kwenye mgogoro na wasanii kibao ambapo wapo walio kubali yaishe kwa kupiga magoti na kuomba msamaha, isipokuwa Lady Jaydee ambaye bado ana vita nao iliyodumu kwa miaka mingi.
Ruby anasema mwisho wa siku ni maisha yake ndiyo ya muhimu zaidi. Ruby alipatikana kupitia shindano la Supa Diva liliondaliwa na Clouds kupitia tamasha la Fiesta na kusainishwa chini ya kampuni ya THT iliyoanzishwa na Ruge Mutahaba.
“To be honest naumia sana sababu they don’t care,” anasema. “So if someone hakujali, what can you do? Tatizo ndio kama hilo unakuwa na management ambayo haijali maslahi yako kwenye maisha yako. Tunajikuta tunakuwa na management ambazo zinajali umabavu, zinaendesha wasanii kimabavu kuliko kiakili ya kutimiza malengo ya wasanii wao ambapo sisi wasanii wa kike tunaonewa sana. Unadhani kwanini Lady Jaydee wanamuita komando?” amehoji Ruby.
“Because ni mtoto wa kike, ni mwanamke ambaye amesimama kweli kweli na kujitetea, lakini wachache sana wanafanya hivyo.”
Kukiwekea kidonda chumvi, Ruby ambaye kwenye Instagram amepost video akiimba wimbo wa Lady Jaydee, amedai kuwa ana mpango wa kufanya naye kazi. “Nitafanya naye sababu ni muimbaji mzuri, ana sauti nzuri.”
Powered by Blogger.