Msanii Nikki mbishi ametoa msimamo wake kuhusu kuchanganya Hip Hop na Singeli,amesema

Baada ya msani wa hip hop,One The Incredible kujitokeza na kusema kuwa hakuna kitu kama Hip Hop Singeli kama anavyodai Mkongwe wa Hip Hop ,Professor Jay kuwa wimbo wake wa Kazi kazini Hip Hop Singeli,Msanii mwingine wa hip Hop,Nikk Mbishi ameendelea kusisitiza kuwa hip hop haiwezi kuchanganywa na kitu chochote.
Akiongea kwenye moja ya mahojiano yake Nikk Mbishi amemtaka Professor kusema kuwa amefanya hip hop na singeli au amefanya Singeli na sio hip hop singeli kama anavyodai.
Hip Hop haichanganyiki na chochote,Hip Hop iko na misingi yake na kila kitu chake na inajitegemea.kwa hiyo unapotaka ku fuse hip hop na kitu kingine itambue kwanza hip hop,Jay anajua, mimi namwitaga Babu, ni father wa hii rap game,lakini hatakiwi kusema amefanya hip hop singeli ,mimi namwambia si kweli.Hiyo ni hip hop na singeli au useme umefanya Singeli” alifunguka Nikk Mbishi.
Powered by Blogger.