Wakati huku nyumbani Tanzania akionekana kama ni msanii aliyefulia, Mr.Nice moja ya wasanii waliowahi kutamba sana nchini bado ni lulu nchini Kenya. Msanii huyo ameweka wazi kuwa maisha yanamwendea poa nchini ambapo kwa sasa amepata dili la kufanya tour kwenye county 47 za nchini Kenya.
Akiongea na Radio One kwenye kipindi cha Dj Show,Mr. Nice amesema licha ya tour amepata maombi kutoka kwa wasanii wakubwa wa kenya ili afanye nao kazi.
Niko huku Kenya,kuna kampuni ya Nigeria imenipa dili la kufanya tour kwenye county zote za Kenya, ziko 47, Pia nina project na wasanii wengine wa Kenya ambao wameniomba nifanye nao kazi,tuko na project na Jaguar na nyingine na Wyre kwa hiyo soon mambo yatakuwa mazuri” alifunguka Mr.Nice

kama wewe ni msanii na ungependa kazi yako ionekane kwenye website hii basi wasiliana nasi kwa namba +255714903603

Facebook Blogger Plugin by Harocq

 
Top