Lebo kubwa ya muziki ya Sony Records wamsajili huyu rapa mwenye miaka 13.

Lebo kubwa ya muziki Epic/Sony records wamefanya usajili mkubwa wiki hii baada ya kupata saini ya rapa Luis Rivera Jr Aka Lil Poopy mwenye miaka 13.


Lil Poopy alikuwa msanii wa French Montana kwenye kundi lake la Coke Boys na kutoa mixtape iliyopewa jina “Coke Aint A Bad Word“.


Album hii ilileta matatizo kwenye familia ya Lil Poopy na baba yake
mzazi kuchunguzwa na polisi baada ya mtoto wake mwenye miaka 13 kuimba
kuhusu Wanawake, dawa za kulevya ,ngono na magari ya thamani.


Msanii huyu anafananishwa na wasanii kama Bow wow,Lil Romeo na Taylor Swift walioanza muziki wakiwa wadogo.

Powered by Blogger.